Wizara ya elimu ikishirikiana na ile ya afya katika kaunti ya Nyamira itapeana dawa za minyoo kwa wanafunzi wa shule za msingi hii leo, Alhamisi. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza na mwandishi huyu wa habari, msimamizi wa afya kutoka kaunti ya Nyamira Charles Mogaka alielezea aina za minyoo wakayotibu. 

“Kuna aina nyingi za minyoo, tuna Askaris, ambayo pia inaitwa Roundworms, tuko na Hookworms na vilevile tuko na Whips. Hizi aina tatu zinatibiwa kwa kupeana dawa aina ya Albendazole ambayo inapeanwa kwa watoto kati ya umri wa miaka miwili hadi kumi na minne," alisema Mogaka.

"Dawa hii ni tembe moja ambayo mtoto anatafuna na kumeza. Pia tuna ugonjwa wa Bilharzia au Schistomiasis vilevile tuko na Haematobium ambao hupitia kwa maji. Mtu ambaye ana minyoo hawa akiweka kinyesi au kuenda haja ndogo kwa maji ya kuogelea vile virusi husalia kwenye maji," aliongeza Mogaka.

Aidha, Mogaka alizidi kubaini kuwa mtu anapokunywa maji yaliyo na mayai ya Bilharzia, anaweza kupata ugonjwa huu. 

Mogaka pia amewasihi wakazi wa kaunti ya Nyamira kudumisha usafi kama njia moja ya kuangamiza minyoo, na ameongeza kusema kuwa ni mhimu kila mkaazi kuhakikisha kuwa ana choo yake pale nyumbani.