Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huku chuo kikuu cha anuwahi cha Mombasa kikitarajiwa kufunguliwa siku ya Juamatatu, wanafunzi wa chuo hicho ambao walifukuzwa wameapa kutolipa zaidi ya shingi elfu mbili ambazo kila mwanafunzi anahitajika kutoa ili kugharimia hasara iliyosababishwa na wanafunzi hao kwenye ghasia zilizosababishwa mwezi jana.

Wanafunzi hao, kupitia kwa katibu wao, Hillary Nyangor, katika kikao na wanahabari siku ya Alhamisi walisema kuwa sharti chuo hicho kizingatie matakwa ya wanafunzi hao na tatizo lililosababisha wao kufanya maandamano, badala ya kuwataka kulipa hela ilhali hawakuhusika katika uharibifu uliofanyika.

Alisistiza kuwa lazima usimamizi wa chuo hicho kuwaita wanafunzi na kuwa na kikao na wao kabla ya kupitisha mazimio bila kuwahusisha wanafunzi ambao ndio waathiriwa.

Alisema kuwa wanafunzi watasusia kurudi chuoni iwapo watahitajika kulipa kiwango hicho cha shilingi elfu mbili, na kumtaka chansela mkuu wa chuo hicho profesa Josephat Mwatella kuweka juhudi za kutafuta mwafaka kati ya wanafunzi na mamlaka ya chuo hicho.

Wanafunzi wa chuo hicho walifanya maandamano mnamo tarehe 19 mwezi uliopita wa Oktoba wakilalamikia kuongezwa kwa pesa flani kwenye karo, ambapo walidai kuwa usimamizi wa shule hukuwahusisha wakati wa kufanya uamuzi huo.

Kisa hicho kilisababisha kuchomwa kwa malori mawili ya kuzoa taka ya Kaunti ya Mombasa, kisa ambacho kiliweza kujadiwa katika bunge la Kaunti hiyo na hata gavana wa kaunti kutaka wanafunzi waliohusika katika kuteketezwa kwa malori hayo kushikwa na kushtakiwa dhidi ya kosa la uharibifu wa mali.