Wanafunzi wote waliopata zaidi ya alama 400 katika mtihani wa darasa la nane mwaka jana katika eneo bunge la Nyaribari Masaba Kaunti ya Kisii watafadhiliwa masomo yao kupitia hazina ya ustawi maeneo bunge CDF ili kuendeleza masomo yao.
Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Keroka, mbunge wa eneo hilo la Nyaribari Masaba Elijah Moindi aliahidi kutoa usaidizi kwa wanafunzi waliopita zaidi ya alama 400 ili kuendeleza masomo yao
Kulingana na Moindi wanafuzi waerevu wa aina hiyo wanastahili kufadhiliwa kimasomo kwani alama walizopata ni za juu zaidi na kuna haja ya kufadhiwa ili waje kusaidia siku sijazo.
“Nimetoa ahadi kwa wanafunzi wote waliopata alama ya zaidi ya 400 katika eneo bunge langu nitawafadhili kupitia hazina ya CDF ili waendelee na masomo,” alisema Moindi.
Aidha, Moindi aliomba wazazi wote katika Kaunti ya Kisii kuwasomesha watoto wao huku akisema masomo ni msingi wa kila jambo maishani na kusema elimu inasaidia.
Matamshi ya mbunge huyo yaliungwa mkono mbunge wa eneo bunge la Borabu Ben Momanyi ambaye alisema kila mtoto anastahili kusomo ili aje kujisaidia siku za usoni.
“Mtoto anaposoma huwa rahisi kujua jinsi nchi inavyoendeshwa na ndio viongozi wa kesho kila mmoja akumbatie masomo kwa moyo mmoja ili eneo la Kisii lifauru na kuuongoza kwa wasomi,” alisema Momanyi.