Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanahabari mjini Nakuru walitenga Krisimasi yao na kujumuika na watoto wa mitaani mjini humo katika bustani ya Nyayo Gardens

Vituo vya redio vya Hero FM, Sauti ya Mwananchi Radio na MBCI vilijumuika na watoto hao na kuwatolea zawadi ya Krisimasi.

“Tulichukua hatua ya kusheherekea na watoto hawa wa mtaani kwa sababu tunafahamu wanachopitia, tunajua pia hawana chochote ambacho wanaweza kusherehekea,” Mc Emo alisema.

Wanahabari hao walihimiza Wakenya haswa wa kaunti ya Nakuru wawajali na kuwasaidia wasiojiweza maishani msimu huu wa krismasi na mwaka mpya.

Vijana pia walishauriwa kujiepusha na anasa na uraibu wa pombe msimu huu wa shamra shamra za sherehe nyingi.

“Vijana wenzangu tafadhali nawaomba tujiepushe na anasa zisizofaa,” Edwin Korobe.