Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanaharakati wa kutetea maslahi ya haki za kibinadamu wameshinikizwa kuzingatia haki za kimsingi na kibinadamu kwa Wakenya kama jinsi katiba ya nchi inavyoangazia ili kuona kwamba maswala ya maendeleo mashinani yanatekelezwa vyema.

Mshirikishi mkuu wa Shirika la vijana wa Kiislam KIMYA ukunda wa Pwani Khamis Juma Mwaguzo amedai kuwa serikali imeonekana kwa kiwango kikubwa ikikiuka katiba ya nchi na kuwanyanyasa Wakenya hali ambayo inachangia kusambaratika kwa maswala muhimu nchini.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Mwaguzo amesema kuwa kuna haja ya serikali kulichukulia swala hilo kwa makini sambamba na kuhakikisha kuwa kila Mkenya anapata haki zake za kimsingi ili haki za kibinadamu kuzingatiwa.

Amewataka viongozi wa kisiasa hasa wabunge wa kitaifa kuwa katika mstari wa mbele kutetea katiba ya nchi ili kuona kwamba haki za kibadamu nchi zinazingatiwa na kuwalinda Wakenya katika maswala mbalimbali ya unyanyasaji ili kuwawezesha kuimarisha uchumi wa nchi.

"Tunaiomba serikali kuzingatia haki za kibinadamu pamoja na vipengele vya katiba ili haki za Wakenya kuzingatia na kuhakikisha kuwa maswala ya kimaendeleo yanatekelezwa," alisema Mwaguzo.

Mwaharakati huyo wa haki za kibinadamu katika eneo la Pwani amesema kuwa lazima swala hilo kuangaziwa vyema na kuhakikisha maswala ya kimaendeleo mashinani yanatekelezwa.