Share news tips with us here at Hivisasa

Wananchi wanaomiliki zaidi ya bunduki mbili watachunguzwa ili kuweka wazi jinsi walivyozipata bunduki hizo jijini Mombasa.

Akitoa kauli hiyo kwenye kikao na wanahabari siku ya Jumanne, kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa alisema kuwa idara ya usalama itawafanyia uchunguzi ili kuweka wazi uahalali wa bunduki hizo, ikizingatiwa wengi wanamiliki bunduki hizo kinyume cha sheria.

Marwa aliongeza kuwa watakaopatikana na bunduki kinyume cha sheria watapokonywa na kukabiliwa kisheria.

Aidha, alionyesha kughadhabishwa kuona kuwa kuna raia wanamiliki zaidi ya bunduki sita jijini Mombasa ambazo amezitaja kutumika na wahalifu kutekeleza uhalifu jijini.

Haya yanajiri baada ya wahalifu wengi kushudiwa wakitumia bunduki ambazo hazijulikani zinatoka wapi jijini Mombasa.