Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Spika wa kaunti ya Nakuru Susan Kihika Ijumaa alisema ni jambo la kusikitisha vijana wa nchi wakiangamizwa na ajali za barabara na vileo wanavyouziwa na watu wasiojali maslahi yao.

Bi Kihika alisema wakati umewadia kila mtu katika jamii awajibike haswa wazazi na walezi wa watoto.

Akihutubia waombolezaji wakati wa mazishi ya wavulana wanne waliofariki mkesha wa mwaka mpya katika ajali ya barabara eneo la Salgaa.

"Aliyewauzia pombe wavulana hao alikosea,” Kihika alisema.

Vile vile alitoa wito hatua ichukuliwe dhidi ya afisa wa polisi aliyewakodisha gari wavulana hao.

Wakati huo huo mamlaka ya usalama na uchukuzi itaanza kupiga darubini shule zinazowapa leseni madereva ambao hawajahitimu.