Wanaume watatu wamefikishwa katika mahakama ya Mombasa kwa madai ya kuhusika katika wizi wa mabavu.
Salim Kimanzi Wambua, Albert Ichami Mkabwa na Dickson Muungu Peter wanadaiwa kutekeleza kosa hilo mnamo Januari 3, 2016, katika eneo la Wayani huko Changamwe wakiwa na wenzao ambao hawakuwa mahakamani.
Aidha, mahakama imeelezwa kuwa watuhumiwa wakiwa wamejihami na mapanga na rungu walimnyang’anya Omondi Gabrieli Amuok pesa taslimu shilingi 15,000 na simu ya mkononi yenye thamani ya shilingi 7,900.
Watuhumiwa walikana madai hayo mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa Nicholas Njagi, na kupewa dhamana ya shilingi milioni tatu kila mmoja.
Kesi hiyo itasikilizwa Februari 9,2016.