Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaume wawili wamefikishwa mahakamani kwa madai ya kupatikana na bunduki na kemikali inayoaminika kutengezea vilipuzi.

Mohamed Mwichande Kombo na Mohamoud Salim Mohamed wanadaiwa kupatikana na bunduki aina ya G3, kemikali ya Acetone na risasi, mnamo Januari 4, 2016, katika eneo la Shikamo huko Majengo.

Wawili hao walikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu Susan Shitub siku ya Ijumaa.

Mahakama itatoa uamzi wa kupewa dhamana yao mnamo Februari 16, 2016.