Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wanaumme wawili wanaodaiwa kuiba shilingi 35,000 huenda watalazimika kusalia rumande hadi mwaka ujao iwapo watakosa baili ya shilingi 20,000 pesa taslimu kila mmoja.

Hii ni baada ya wawili hao; Alfred Mboto na George Kuria kukana shtaka hilo baada ya kufikishwa mahakamani hii leo Alhamisi kujibu shtaka hilo.

Upande wa mashtaka uliarifu mahakama ya Nakuru kuwa Mboto na Mwaura walimwibia Mary Nduta Karanja shilingi 35,000 wakishirikiana na wengine ambao hawakuwa mahakamani kati ya tarehe 8 Septemba mwaka huu na tarehe 27 Oktoba mwaka huu mjini Nakuru.

Washtakiwa hao walikana shtaka hilo mbele ya hakimu mkuu Alice Chemosop Towett wa mahakama ya Nakuru, ambaye aliwaachiliwa kwa baili ya shilingi elfu ishirini pesa taslimu kila mmoja.

Kesi hiyo sasa itatajwa Novemba tarehe kumi mwaka huu na kuskizwa Januari 21 mwaka ujao.