Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaume wawili wametiwa mbaroni wakiwa na gunia moja ya bangi katika kituo cha magari mjini Kisii.

Wanaume hao walikabiliwa na maafisa wa polisi siku ya Alhamisi baada ya wananchi kupokeza maafisa wa polisi habari hiyo huku wakiwa na nia ya kusafirisha bangi hiyo kuelekea mjini Keroka.

Akitibithisha kisa hicho, mkuu wa polisi wilayani Kisii ya kati Gabriel Gatua alisema maafisa wa polisi walipokezwa habari hiyo na wananchi, kisha baadaye waliwatia mbaroni washukiwa hao.

“Washukiwa hao wa madawa ya kulevya tayari wametiwa mbaroni na wako katika kituo cha polisi cha Kisii wakisubiri kufikishwa mahakamani,” alisema Gatua.

Katika kituo cha magari mjini Kisii, madawa ya kulevya yamekuwa yakiuzwa kwa muda mrefu pamoja na pombe haramu, huku baadhi ya wafanyibiashara wa mboga wakijifanya kuuza mboga ili hali huuza pombe na madawa hayo ya kulevya.

Gatua aliomba wananchi kuendelea kuwasaidia kwa kuwapokeza habari wanaposhuhudia watu wa aina hiyo wakifanya biashara hizo ambazo si halali nchini.