Miili ya Wanaume wawili wa umri wa makamo ilipatikana katika mto wa Nyansangio lokesheni ya Mugirango kaunti ya Nyamira.
Miili ya wawili hao ilipatikana mnamo siku ya Jumanne ikiwa na majeraha mabaya huku ikiwa imeondolewa macho.
Akitibithisha kisa hicho, chifu wa lokesheni hiyo Dancan Moriasi alisema wawili hao hawajulikana wanakotoka na kusema huenda waliuawa katika sehemu tofauti huku miili yao ikitupwa katika mto huo wa Nyansiangio.
“Hawa watu hawatoki katika sehemu yetu hapa maana hatuwajui na huenda waliuawa katika sehemu tofauti kisha baadaye wakaletwa na kutupwa hapa ,” alisema Dancan Moriasi, chifu wa lokesheni ya Mugirango .
“Lakini tumeanzisha uchunguzi ili kubaini ni wapi wanakotoka ili ukweli ujulikane na yeyote ambaye amekosa mwenzao tunamuomba aje ajaribu kuwatambua,” aliongeza Moriasi.
Katika kaunti ya Nyamira visa vya mauaji kiholela yamekuwa yakishuhudiwa kila kuchao huku wakazi wakiomba kuimarishiwa usalama wao kwani idadi kubwa inahofia maisha yao.