Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanawake watano kutoka vijiji vya Nyaisa na Manga wilayani Manga kaunti ya Nyamira walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la kuwakeketa watoto wao kinyume cha sheria.

Watano hao walifikishwa katika mahakanama ya Nyamira siku ya Jumanne na kushtakiwa mbele ya jaji wa mahakama hiyo RM Gitagwa. Jaji huyo alisema ni kinyume cha sheria kuwakeketa watoto wasichana .

Watano hao ni Beatrice Kemunto, Caroline kerubo, Teresa Kwamboka , Ebisbar Kerubo na Christine Beta.

Visa vya ukeketaji vimekuwa vikiripotiwa kwenye eneo hilo licha ya kuwa serikali imeonya kuhusu mila hio.

“Wasichana hawastahili kutahirishwa kulingana na sheria na unapomtahiri mtoto msichana ni kumdhulumu na kukiuka sheria,” alisema jaji R.M Gitagwa.

Watano hao waliachiliwa kwa bondi ya shillingi 50,000 kila mmoja huku kesi hiyo ikitajiwa kusikizwa tena tarehe Februari 7, 2016.