Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Idara ya trafiki katika eneo la Pwani imewataka abiria wanaosafiri msimu huu wa Krismasi kuwa waangalifu na makini ili kuepuka kulaghaiwa na wakora wanaojifanya wahudumu wa mabasi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya Jumatatu, meneja wa dharura katika idara ya trafiki eneo la Pwani Solomon Njuguna, aliwahimiza abiria kutembelea vituo vya kuabiri magari ambavyo vinatambulika na serikali wanapotaka kusafiri.

Njuguna alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia abiria kuepuka kukatiwa tiketi bandia na walaghai ambao wanalenga kuvuna kwa njia ya haramu.

Aidha, amewataka abiria hao kupiga ripoti kwa idara ya usalama iwapo watashuhudia visa vyovyote visivyo vya kawaida katika vituo vya kuabiria magari.

Afisa huyo pia ametoa onyo kali kwa madereva wenye mazoea ya kuendesha magari kwa kasi, kwa kusema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria iwapo watapatikana na hatia.