Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali imetakiwa kuweka mfumo bora wa kuhakikisha kila msanii hapa nchini analipa ushuru.

Akizungumza siku ya Jumatano, msanii Herman Gakobo Kago maarufu kama Profesa Hamo alisema ya kwamba wasanii wanawajibu wa kuchangia katika ukuaji wa maendeleo na uchumi wa nchi hii.

Alisema kuwa wasanii wanaokwepa kulipa ushuru , wanafaa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Msanii huyo ambaye ni mkaazi wa kaunti ya Nakuru na ambaye amekuwa akitia fora katika kipindi cha televisheni cha Churchill Show kwenye runinga ya NTV, alisema kuwa ingawa wasanii wengi wamepata na kupokea talanta kutoka kwa mwenyezi mungu bila malipo, wanafaa pia wachangie kwa jamii na kwa taifa mapato wanayopata.