Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaume wanane wamehukumiwa kifo kwa kosa la mauaji ya Kahindi Ngawa Katana kwa tuhuma za uchawi mwaka 2012 huko Matonomane.

Safari Foleni Ngawa na wenzake saba wanadaiwa kumkatakata kwa mapanga mwendazake mnamo Julai 21, 2012, kwa kisingizio cha uchawi katika eneo la Matonomane huko Kilifi

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumanne, jaji Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha wazi kuwa wanane hao walihusika katika mauaji hayo ikizingatiwa wote wanatoka katika familia moja.

Muya aliongeza kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wote wanajihusisha na mauwaji ya kiholela nchini.

Washtakiwa wako na siku 14 za kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.