Share news tips with us here at Hivisasa

Wasichana wanne wanaokabiliwa na madai ya kuhusika katika ugaidi wamefunguliwa mashta mengine mapya ya kujaribu kupanga kutekeleza ugadi nchini.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama siku ya Ijumaa kuwa mnamo Machi 26, 2015, Ummulkheir Sadri Abdalla, Khadija Abubakar Abdulkadir, Maryam Said Aboud na Halima Adan, wanadaiwa kufanya mkutano jijini Nairobi, kupanga njama ya kutekeleza shambulizi la kigaidi.

Shtaka jingene ni kuwa Ummulkheir Abdalla na wengine kutoka mataifa ya nje walipanga kutekeleza shambulizi la kigaidi katika eneo la El-Wak.

Hakimu katika mahakama ya Mombasa, Simon Rotich aliwanyima wasichana hao dhamana na kuagiza kesi hiyo kusikiliza Machi 9 na 10, 2016.

Wasichana hao wanakabiliwa na kesi nyingine, ambapo walishtakiwa kwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabab, katika mahakama hiyo ya Mombasa.

Wanne hao watasalia katika gereza la Shimo la Tewa.