Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wasiwasi umeshuhudiwa mjini Nakuru baada ya madai ya kuwepo kwa kundi haramu la Mungiki mjini Nakuru kuibuka.

Uvumi huo ulianza baada ya wafanyibiashra wawili mjini humo kutoweka na kasha kupatikana wameuawa na kutupwa kwenye msitu wa Gakoe kaunti ya Kiambu.

Habari zinasema kuwa wawili hao, Joseph Chege na Schem Wachira, walikuwa ni viongozi wa kundi la Mungiki.

“Hao walikuwa viongozi wao (Mungiki) na ndio walitumika kuhangaisha wachuuzi hapa. Sisi kama wachuuzi tumeteseka sana kwa sababu ya kundi hilo,” mchuuzi mmoja alisema.

Aidha mwanasiasa mmoja katika serikali ya kaunti amehusishwa na kundi hilo baada ya kuhudhuria mazishi ya washukiwa hao wa Mungiki.

Wakaazi walisema wana wasiwasi kuwa huenda kundi hilo linachipuka tena na kuanza kuwahangaisha.

“Tunaomba polisi wakabiliane na wao kabisa,” Jane Nyakio alisema.