Huku mitihani ya kitaifa ya KCPE ikiendelea kote nchini, watahiniwa katika Kaunti ya Mombasa wameonya kutokubali kulaghaiwa na baadhi ya watu fulani na kushiri udanganiyifu.
Akitoa wito huyo katika eneo la Kisauni mjini Mombasa siku ya Jumanne, Kiongozi wa vijana katika eneo hilo Maxwell Masai alisema kwamba lazima wanafunzi wawe makini ili kuorodhesha matokea bora katika mitihani hiyo.
Kulingana na Masai, visa vya hivi majuzi vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne ya KCSE ni dhihirisho wazi kwamba sekta hiyo inakumbwa na changamoto.
“Baraza la mitihani nchini linafaa kuibuka na mbinu mbadala za kuzuia udanganyifu katika siku za usoni,” alisema Masai.
Masai aliwataka watahiniwa hao kujitahidi zaidi kuibuka na matokea bora ili Kaunti ya Mombasa iingie katika orodha ya kaunti bora zaidi nchini.
“Ningependa kuwaonya watahiniwa dhidi ya kushiriki udanganyifu kwani ni kinyume cha sheria. Wanafunzi lazima wawe makini ili wawezekufanya vyema,” alisema Masai.
Mitihani hiyo ya kitaifa ya KCPE imeingia siku yake ya pili kuhu baraza la mitahini nchini likishikilia kwamba atakayepatikana akishiriki udanganyifu katika mitihani hiyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.