Mwenyekiti wa shirika la Nacada John Mututho amewaonya wanaoshuhudia watoto wakibugia vileo bila ya kuchua hatua yoyote kwamba watakabiliwa kisheria.
Akizungumza kwenye ibada ya misa ya wafu ya mmoja wa vijana waliaoaga dunia kwenye ajali iliyotokea mkesha wa mwaka mpya katika eneo la Salgaa, iliyofanyika katika eneo la Kikapu siku ya Jumanne, Mututho alisisitiza kwamba yeyote atakayepatikana kwenye eneo ambalo watoto wanabugia vileo atakamatwa pamoja na wale wote ambao watakuwa kwenye klabu hiyo.
Wakati huo huo, amewataka Wakenya kuombea Kenya haswaa wakati huu ambapo tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.
Mututho alisisitiza kwamba uchaguzi unafaa kuwa wa amani huku akiwataka wote kuheshimiana na kuzingatia upendo.
Vijana walioaga dunia ni pamoja na Kevin Kamuru, 19, Bill Kamau, 16, Brian Kariuki, 17, Derrick Mbugua,18, na Dominic Mwangi aliyekuwa akifanyiwa ibaada ya misa ya wafu.
Tayari afisa mmoja wa polisi wa utawala anayefahamika kama Julius Kioko amesema kwamba gari lililosababisha maafa ya vijana hao lilikuwa lake.
Ingawa inadaiwa kwamba vijana hao walikuwa wamekodishwa gari hilo, Kioko alidai kwamba ni rafiki yake aliyewapa vijana hao gari hilo.