Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaume watatu walifikishwa katika mahakama ya Winam jijini Kisumu kujibu shtaka la kuiba ng’ombe watano.

Mahakama iliambiwa siku ya Alhamisi, kuwa watatu hao, Kevin Otieno, Edwin Otieno na Wycliffe Aura, wanadaiwa kuiba ng’ombe hao wenye thamani ya shilingi elfu 150, mali ya Seline Angeline.

Washukiwa hao, wanadaiwa kutekeleza wizi huo katika boma la mlalamishi katika eneo la Wathorego, Kaunti ya Kisumu, mnamo tarehe Septemba 13, 2013.

Watatu hao walikanusha mashtaka dhidi yao.

Mahakama iliagiza waendelee kuzuiliwa, huku upande wa mashtaka ukiendesha uchunguzi zaidi dhidi yao.