Watoto wachanga mpaka wale wenye miaka mitano wamo katika hatari ya kuugua ugonjwa wa utapia mlo kwa mujibu wa daktari wa watoto katika hospitali moja mjini Mombasa.
Akiyazungumza haya katika eneo la Shika Adabu, daktari huyo amesema kuwa wazazi wengi hawazingatii afya za watoto wao hata wanapowapeleka kliniki ya kila mwezi.
"Wazazi hawa huwa hawaulizi ushauri wa vyakula bora kwa watoto na pia hawazingatii kupimwa kama wana virusi vya ukimwi ili kupata huduma bora na dawa za kinga kwa watoto," aliendelea kusema.
Daktari huyo ameelezea wasi wasi wake na kuongeza kuwa watoto ambao wana uzani mdogo kushinda miaka yao ni bora wazazi wao kuwachukulia chakula cha kuboresha afya humo hospitalini.
Takwimu za hospitalini hiyo zinaonyesha kuwa watoto wengi walio chini ya umri wa miaka mitano hawapati lishe inayofaa.