Share news tips with us here at Hivisasa

Watu wanne wamejeruhiwa baada ya mzozo kutokea kati ya jamii mbili (Maasai na Kalenjin), zinazoishi katika kaunti ya Narok na kupelekea zaidi ya familia mia nne sitini kuhama makwao.

Akizungumza na mwandishi huyu jumamosi hii jioni, mratibu wa eneo la bonde la ufa Osman Warfa amesema kuwa mzozo ulizuka baada ya watu wawili wanaoishi katika kaunti hiyo kuuawa siku kadhaa zilizopita katika kaunti hiyo ya Narok.

Ingawa nyumba kadhaa zimechomwa pia kutokana na mizozo ya ardhi katika eneo hilo, amedhibitisha kuwa hadi kufikia sasa polisi wa kupambana na ghasia wa gsu zaidi ya mia mbili wako katika eneo hilo ili kutuliza na kudhibiti hali.

Aidha mratibu wa shirika la msalaba mwekundu katika kaunti ya Nakuru James Gichimo amesema kuwa waliyofurushwa wakiwemo wanawake ,wazee na watoto wamepiga kambi katika shule ya msingi ya Olenguruone township kaunti ya Nakuru.

Aidha ameongeza kuwa miongoni mwa wle waliyojeruhiwa, wawili wamepelekwa katika hospitali ya Tenwek kaunti ya Bomet, mmoja akipelekwa katika hospitali ya Olenguruone huku mmoja akiruhusiwa kwenda nyumbani.

Kadhalika mratibu huyo wa shirika la msalaba mwekundi wa kaunti ya Nakuru ameongeza kuwa watu hao wanahitajki kwa dharura msaada wa kibinaadamu ikiwemo vyakula, vyandarua, nguo maji na hata mablanketi ili kuweza kuwasitiri.

Hata hivyo Gichimo ametoa wito kwa wasamaria wemo kushirikiana nao na kutoa usaidizi wao ili kuweza kuisaidia idadi hiyo kubwa ya watu wanaohitaji misaada.