Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Watu wawili wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya jimbo la Nakuru, baada ya kufunikwa na mchanga kwenye mtaro wa jengo waliokuwa wakichimba msingi wake katikati ya mji wa Nakuru siku ya Alhamisi.

Wawili hao walikuwa wamepoteza fahamu wakipelekwa hospitalini.

Manusura hao walikuwa miongoni mwa vibarua wengine 20, ambao walitoroka walipoona mchanga huo unakatika, na kuwafunika waliokuwa wakichimba.

Hata hivyo, kulingana na naibu OCPD wa Nakuru Janet Wasike, ni kuwa kwa ushirikiano wa maafisa wa polisi sawia na maafisa kutoka kwa shirika la msalaba mwekundu ulifanikisha kuokolewa kwa wawili hao.

“Wananchi waliitika kwa haraka, serikali ya kaunti, polisi na msalaba mwekundu na kufukua wawili hao wakiwa bado hai japo walipoteza fahamu,” Wasike alisema.

Tukio hilo lilitokea karibu na ofisi kuu za kaunti ya Nakuru, nyuma ya jengo la kampuni ya kusambaza umeme nchini KPLC.