Wakenya wametakiwa kuonyesha uzalendo kwa kutobaguana kidini huku Papa mtakatifu ambaye ni koani mkuu wa waumini wa dini ya kikatholiki akitarajiwa kuwasili nchini kwa mara ya kwanza mwisho wa mwezi huu wa Novemba.
Waumini wa dini ya Kiislamu na wale wa dini ya kikiristo wameombwa kuiombea nchi na kushikana mikono na kuinua amani na umoja miongoni mwa wananchi.
Akiongea na waandishi wa habari katika jiji la Mombasa siku ya Jumatano, mshirikishi mkuu wa Jumuia ya Wahubiri na Maimam, CIPK, kwa waumini wa dini ya kiislamu nchini Sheik Mohamed Khalifa aliwataka wakazi wa Mombasa na umma wote kwa jumla kote kila Kaunti kuwapuuza viongozi wa kisiasa ambao nia yao ni kuwatenganisha wakenya kwa azimio la kutaka mamlaka kwa mbinu haramu.
Kiongozi huyo alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wananchi, hasa vijana, kuzingatia elimu na ushauri wa kidini ambao wanapewa na viongozi wa makanisa na wale wa msikiti ili kujiepusha na fujo ambazo zitaitumbukiza nchi hii katika zogo la maafa kama yale yaliyoshuhudiwa mwaka wa 2oo8.
Mwito huu unakuja huku viongozi wa kisiasa wakiwataka wananchi kujiepusha na mikutano ya wanasiasa ambao wanahubiri chuki na matamshi ya kikabla kama ya hivi karibuni kutoka kwa gavana wa Kiambu William Kabogo na aliyekuwa meya wa jiji la Nairobi George Aladwa.