Wanaofanya biashara ya pombe haramu na uuzaji wa madawa za kulevya katika kaunti ya Uasin Gishu wameonywa kwamba watachukuliwa hatua kali.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano na vitengo mbalimbali vya kukabiliana na dawa za kulevya Jumatatu, kamishna wa kaunti hiyo Abdi Hassan amesema kuwa kaunti bado inaendeleza msako dhidhi ya wahusika wanaoendesha biashara hiyo haramu.

"Bado tunapambana na vita hivi, na tutahakikisha wafanyi biashara hao haramu wameondolewa katika kaunti hii," alisema Hassan.

“Wafanyibiashara hao wamezindua mbinu mpya kuuza bidhaa hizi haramu, tunaahidi kukabiliana nanyi," aliongeza Hassan.

Hassan alisema kuwa wanajaribu kupiga msasa mbinu mwafaka ya kukabiliana na janga hilo.

"Mwaka uliopita tulikabiliana na mihadharati vilivyo, lakini mwaka huu tumeona kuwa biashara hiyo imeanza kusambaa tena, hii leo tumekutana ili kupiga msasa vita dhidhi ya mihadarati," alisema Hassan.

Katibu wa kaunti ya Uasin Gishu Peter Lelei alisema kuwa serikali ya kaunti hiyo imetenga bajeti ya kutosha ili kukabiliana na vita hivyo.

Mkutano huo uliwahushiwa maafisa wa usalama, machifu, viongozi wa kaunti na washika dau wengine wanaohusika na vita dhidhi ya madawa ya kulevya.