Wawakilishi wa wanawake wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuinua vipaji na biashara za wanawake maskini mashinani.
Kauli hii ilitolewa na mwenyekiti wa chama cha Maendelea ya wanawake katika Kaunti ya Mombasa Afiya Rama siku ya Ijumaa.
Rama alisema kuwa wanawake wengi mashinani huwa hawanufaiki na miradi ya maendeleo, hali inayowafanya kuzidi kuishi katika lindi la umaskini.
Aidha, alisisitiza kuwa iwapo wanawake watapewa ujuzi na fedha za kufanya biashara, kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa kiwango cha umaskini nchini.
Hatua hii inajiri baada ya wanawake wengi kuhamia mijini na kuendeleza biashara ya kuombaomba na wengine kujihusisha na ukahaba hasa katika eneo la Sabasaba jijini Mombasa.