Kila wadi katika kaunti ya Nakuru itapokea shilingi milioni moja kufadhili elimu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa Nakuru Kinuthia Mbugua alisema kuwa fedha hizo ni katika juhudi za kupiga jeki sekta ya elimu.

Aliongeza kuwa mtoto yeyote hafai kukosa elimu kwa kukosa karo.

"Kila mtoto ana haki ya kupata elimu kwa mujibu wa katiba,"Mbugua alisema.

Alitoa wito kwa wawakilishi wadi kaunti ya Nakuru kuhakikisha fedha hizo zinawafaidi wanafunzi wote wasiyojiweza.