Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wawakilishi wateule wanaoshiriki dini ya kiislamu kwenye bunge la kaunti ya Nakuru wamekariri kwamba hawabaguliwi kwenye bunge hilo la kaunti ya Nakuru.

Wakizungumza na mwandishi huyu Alhamisi mjini Nakuru, wawakilishi hao wateule walikariri kwamba spika wa bunge la kaunti ya Nakuru anawaheshimu na kuwakubali bila ya kuzingatia dini yao.

Mmoja wa wawakilishi hao wateule hao Ruth Jeptarus anayetembuliwa kama Asha kwa jina la kiislamu amefichua kuwa kwa wakati mmoja, spika huyo alikuwa amemwelezea mwakilishi mwenzake mteule katika kaunti ya Nakuru aitwaye Hawa Ibrahim kuwa atawatengea chumba cha kuwawezesha kusali kwa muujibu wa dini ya kiislamu.

Cheptarus kwenye mahojiano ya kipeke na mwandishi huyu mjini Nakuru sasa anataka waislamu wengine kutobaguliwa, sawia na wawakilishi wateule waislamu kwenye bunge la kaunti ya Nakuru wanavyoheshimiwa.

Amewahimiza waalimu pia kuwakumbatia watoto wa dini zote shuleni.

Izingatiwe kuwa kulingana na katiba ya Kenya, hakuna anayefaa kubaguliwa kwa misingi ya kidini, kikabila au kwa misingi yeyote ile.