Share news tips with us here at Hivisasa

Wanaume wawili wamefikishwa kwenye mahakama ya Nakuru kwa madai ya wizi wa pembe mbili za ndovu zenye thamani ya shilingi elfu mia tano kila moja, mali inayomilikiwa na shirika la wanyamapori hapa nchini KWS.

Wawili hao Andrew Jegon Kipruto na Joseph Karani Orego waliofikishwa mahakamani Ijumaa wanadaiwa kutekeleza kosa hilo mnamo tarehe ishirini na nane Januari mwaka huu mwendo wa saa saba za mchana.

Mahakama imeelezwa kwamba wawili hao walinaswa na pembe hizo katika mzunguko wa uwanja wa maonyesho wa kilimo mjini Nakuru.

Hata hivyo walikanusha shtaka hilo mbele ya jaji wa mahakama hiyo Liz Gicheha.

Kesi hiyo sasa itaskizwa Februari 1.