Masomo katika shule zote za umma eneo la Maella mjini Naivasha yameendelea kuadhirika kwa wiki ya pili sasa, huku wanafunzi wakikosa kwenda shuleni, baada ya mzozo kuibuka.
Wazazi waliandamana wakilalamikia hali hiyo wakitaka serikali iingilie kati mzozo huo, ambapo waliwatoa wanafunzi wao shuleni.
Kamishna wa kaunti ya Nakuru Joshua Nkanatha siku ya Jumanne aliagiza kufunguliwa kwa shule hizo Jumatatu 15,Feb, 2016.
Licha ya serikali kuagiza kuwa shule zote zifunguliwe, wazazi wamekaidi amri hiyo japo hali ya utulivu imerejea eneo hilo.
Mkuu wa elimu wilayani Naivasha Mbugua Kabaki alisema kuwa hakuna masomo yaliyokuwa yanaendelea eneo hilo.
“Tulitangaza hata kwenye makanisa na sehemu zingine kwamba wazazi warejeshe watoto shuleni leo Jumatatu, lakini amri hiyo imepuuziliwa mbali” akasema Kabaki.