Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme mmoja na mkewe wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100, 000 na mdhamini wa kiasi sawa kama hicho au pesa taslimu shilingi elfu 50 kwa shtaka la kumwoza binti yao mwenye umri mdogo.

Washtakiwa hao, Samir Mohammed na Munira Said wanadaiwa kumwoza binti yao mwenye umri wa miaka 14 mnamo Disemba tarehe 24, 2015 huko Kibokoni kaunti ya Mombasa.

Washtakiwa walikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu mwandamizi Richard Odenyo wa mahakama kuu ya Mombasa.

Kesi hiyo itasikizwa tena mnamo tarehe Machi 22, 2016.