Bodi ya Uainishaji wa filamu nchini Kenya (KFCB) imetoa wito kwa wazazi kuchunguza filamu na michezo ya video ambayo watoto wao wanatizama.
Bodi hiyo ya kudhibiti filamu nchini imesema kuwa makundi ya kigaidi yanaweza kutumia majukwaa hayo kuwasajili watoto.
Mkurugeni mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema kuwa vijana wengi wanasajiliwa na makundi hayo haswa wakiwa likizoni.
"Tuko mbioni kufanya mazumgumzo ili kuokoa watoto ambao wamesajiliwa na magaidi kupitia video," alisema Mutua kupitia ukurasa wa Facebook.
Mutua pia alitoa wito kwa vyombo vya habari kwa jumla kudhibiti sawasawa vipindi wanvyoweka hewani, wakidai kuwa wamepata malalamishi kutoka kwa wazazi.
"Filamu ambazo hazifai hazitakubaliwa kupeperushwa hewani. Sheria hii isidhaniwe kuwa ni ya kunyima vyombo vya habari uhuru wao," aliongeza.