Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazazi jijini Mombasa wametakiwa kuungana na kupiga vita jinamizi la dawa za kulevya ili kuokoa vizazi vijavyo kutokana na jinamizi hilo.

Kauli hii ilitolwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir siku ya Jumamosi jijini Mombasa.

Nassir alishutumu wazazi wanaolekeza vidole vya lawama kwa viongozi kwa kuharibika kimaadili kwa watoto wao, na kusisitiza kuwa wazazi ndio wanawapendekeza watoto wao kupotea katika maadili bora.

Abdulswamad aidha alieleza kuskitishwa kwake na ripoti ya kuwa takribani asilimia 98 ya watumizi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Mombasa ni waislamu, jambo linalorudisha nyuma vijana.

Kauli yake iliungwa mkono na Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi kwa kusisitiza kuwa ni lazima wazazi kuwajibika juu ya familia zao ili kuepuka kuharibika kwa watoto.