Wazazi wa eneo la Kisauni wametakiwa kuwajibika pakubwa katika kuwakinga watoto wao kujiunga na kundi haramu la 'Wakali Kwanza'.
Kauli hii ilitolewa na kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa Francis Wanjohi siku ya Jumatano, na aliongeza kusema kuwa Kundi la wakali kwanza linachangiwa na wazazi kutowajibika na watoto wao kama kutojua pale wanapotoa pesa kufadhili kundi hilo.
Aidha, aliwataka wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao hasa marafiki zao ili kupunguza visa vya uahalifi sehemu hiyo.
Vile vile alisisitiza kuwa serikali haitowasaza iwapo hawatajisalimisha na kukoma kuwaangaisha wananchi.
Wakati huo huo, Wanjohi pia amewataka vijana kutojiunga na vuguvugu la MRC kwa kisingizio cha ukosefu wa kazi kwani kuna mbinu mbadala wanaweza tumia kujikimu kimaisha.
Juma lililopita, vijana wawili wa kundi hilo walipigwa risasi na kufariki walipokuwa wakitekeleza uahalifu eneo la Kisauni.