Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazee wa jamii ya Agikuyu chini ya mwavuli wa Baraza la Wazee Bonde la Ufa, sasa wanamtaka raisi Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kutatua mizozo ya mashamba katika kaunti ya Nakuru, ambayo imeripotiwa kuongezeka hivi karibuni.

Wakizungumza na wanahabari mjini Nakuru mnamo Alhamisi na kuongozwa na mwenyekiti wao Gilbert Kabage, viongzi hao walisema amani katika kaunti ya Nakuru na mkoa wa Bonde la Ufa imeanza kuzorota kutokana na wabinafsi kunyakua mashamba ya wengine.

“Kaunti ya Nakuru mizozano hii ya mashamba imepita mipaka. Juzi Mohamed Swazuri ametoka kusuluhisha mzozo wa shamba la Barina Rongai, na sasa mizozo mingine imechipuka katika shamba la Utheri wa Lari na Ngongongeri,”Kabage alisema.

Alisema kwamba serikali haina budi kulinda raia na mali yao kwa mujibu wa katiba.

“Tunamtaka rais Uhuru Kenyatta, waziri Joseph Nkaissery, mkuu wa polisi Joseph Boinet kwa ushirikiano na mwenyekiti wa NLC Mohamed Swazuri, waingilie kati kumaliza mizozo hii katika kaunti yetu,” aliongeza Kabage.