Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa kuzima moto katika kaunti ya Kisii wamelaumiwa kwa kutowajibikia kazi yao inavyostahili.

Hii ni baada ya vibanda vya wafanyibiashara katika eneo la Mwembe viungani mwa mji wa Kisii kuteketea siku ya Jumatano bila afueni kutoka kwa maafisa hao wa kuzima moto.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano katika eneo la Mwembe, mmliki wa vibanda hivyo vlivyoteketea Richard Ondieki alisema aliwapigia simu maafisa hao wa kuzima moto ili kuokoa mali yaliyoteketea na kuchukua muda mrefu kufika.

Aidha, Ondieki alisema wazima moto hao walipofika hawakuwa na maji na kulazimika kuenda kuleta maji kutoka eneo la Kegati, na waliporudi wakapata mali yote imeteketea.

“Hawa wazima moto wa kaunti ya Kisii hawawezi saidia mali inapoteketea maana wanapoitwa huchukua muda mrefu na hawakuangi na maji,” alisema Ondieki.

Aidha, Irene Kerubo na Zipporah Onsarigo walisema kuwa wazima moto hao hawana ujuzi wa kutosha kwani hawajui mahala pa kuanzia wanapozima moto

Sasa wakazi hao wanaiomba serikali ya kaunti kuwapa mafunzo ya kutosha wazima moto hao ili kuwa na ujuzi wa kuzima moto ili kuokoa mali wakati wa mikasa.