Waziri wa Afya katika Kaunti ya Nakuru Dkt Mungai Kabii amewaonya wanaofuzu kutoka vyuo vikuu dhidi ya kupeana hongo ili kupata ajira. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza wakati wa kufuzu kwa wauguzi katika shule ya kutoa mafunzo ya wauguzi ya PCEA Nakuru magharibi, Dkt Kabii anasema kuwa swala hilo ni ufisadi na unafaa kukomeshwa. 

"Wakati ni sasa kukomesha swala hilo katika jamii na taasisi za elimu, tupunguze visa vya kupeana hongo ndio tupate ajira," alisema Kabii.

Wakati huo huo, waziri Kabii amesema kuwa Kaunti ya Nakuru itaendelea kuajiri wale ambao wana tajriba katika sekta ya afya ili kuimarisha utendakazi. 

Hata hivyo, ametoa wito kwa kila mmoja katika jamii kushirikiana katika kutokomeza ufisadi kwenye sekta ya afya. 

Wauguzi 59 walifuzu kutoka shule hio ya uuguzi ya PCEA Nakuru magharibi.