Madereva wa magari ya kusafirisha abiria mjini Nakuru wameelezea furaha yao kutokana na kuimarika kwa biashara siku tatu kabla ya siku kuu ya krismasi. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Shughuli za usafiri wa umma mjini Nakuru zimeshika kasi huku mamia ya abiria wakisafiri kuelekea maeneo mbalimibali kujumuika na jamaa na marafiki wao kusherehekea krismasi. 

Baadhi ya madereva waliozungumza na mwandishi huyo walisema kuwa abiria wameongezeka, na kuwa hawana budi kupandisha nauli. 

Peter Ndegwa, ambaye ni dereva wa magari ya Mololine Shuttle amesema kuwa ongezeki la abiria ni furaha kwao kwani ni wakati wao wa kuvuna. 

"Sisi kama madereva tunafurahia wakati abiria wanapokuwa wengi kwa sababu hatukai sana kwenye steji na magari yanajaa haraka sana," alisema Ndegwa. 

"Nauli itapanda kwa sababu lazima tufidie ule muda tutapoteza barabara ni kutokana na msongamano wa magari," aliongeza.

Ndengwa hata hivyo ametoa wito kwa madereva wenzake kuwaheshimu abiria na kuwahudumia kwa taadhima na heshima kuu.