Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wenyeji na wafanyabiashara katika barabara ya Mnazi Mmoja eneo la Mbaraki wametoa wito kwa halmashauri ya kusimamia barabara za mjini nchini kuweka matuta katika barabara hiyo ili kuzuia visa vya ajali ambavyo vimekuwa vishuhudiwa kwa siku za hivi karibuni.

Wamesema kuwa barabara hiyo kwa muda mrefu imekuwa na visa vya kutamausha vya watu kugongwa na magari na kufa papo hapo, na hamna hatua yoyote kufikia sasa imechukuliwa kuzuia visa hivyo.

Wameongeza kulaumu wenye magari makubwa kwa kuwa na mbinu mbaya za kupeleka magari yao vibaya, na kuwa mara nyingi hudharau watu wa kuvuka barabara, wenye baiskeli pamoja na wendeshaji wa pikipiki.

Shaniez Rashid, ambaye hutumia barabara hiyo wakati mrefu akielekea kazini, amestajabishia visa kama vitatu ambavyo ameshuhudia moja kwa moja watu wa kutembea kwa miguu kugongwa na malori ambayo hutoka eneo la Likoni Bandarini.

Naye Jesephat Mwema, ambaye ni mchuuzi amewalaumu madereva wa magari ambayo huonekana kuendesha magari kwa kasi mno, hali ambayo alisema imekuwa ikichangia sana visa vya maafa na ajali ambazo zinaweza kuepukika iwapo matuta yangekuwa yameundwa.

Kwa sasa wanaitaka idara ya trafiki kushuglkia swala hilo, na kuhakikisha visa hivyo vinapunguzwa kwa kiasi kikubwa. 

Haya yanajiri siku moja tu baada mwendesha pikipiki mmoja na abiria wake kugongwa na abiria huyo kufa papo hapo na mwenzake kuachwa na majeraha mabaya zaidi baada ya lori moja lililokuwa likitoka bandarini kuwagonga.