Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wenye biashara na wenyeji katika eneo bunge la Mvita wameshtumu kisa cha dereva mmoja kumgonga na kumuua mtu mmoja ambaye inasemekana kuwa na akili punguani, na kuitaka idara ya usalama kumtia nguvuni na kumshataki dereva huyo.

Wakazi hao wa eneo la Bouxton wameshtumu vikali uendeshaji wa kiholela wa matatu za kuenda Bamburi ambazo zimesababisha kifo cha punguani mmoja siku la Jumatatu.

Wakazi hao walizishtumu matatu za kutoka kati kati ya jiji kuu la Mombasa kwa kutojali usalama wa watu, na mara kwa mara kupuuza sheria za trafiki hali ambayo imeshuhudia visa vya vingi vya ajali.

Wakiongozwa na Shari Mwambi, wakazi hao pamoja na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo la Bouxton waliongeza kuwa sharti serikali ishirikiane na idara ya mashtaka kwa umma kutia nguvuni dereva huyo .

“Huyu aliyemgonga ni mmoja wa madereva wajeuri wa ‘route’ ya Bamburi na alitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo, na marehemu alikuwa jamaa wa kuomba kutoka kwa wapita njia na tayari alikuwa na upungufu, akili yake si sawa,” alisema mkazi huyo.

Marehemu alipekekwa katika hifadhi ya hospitali kuu ya Pwani, na dereva aliyesababisha ajali akatoroka.