Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Majambazi wawili waliokuwa wamejihami na bunduki wamelivamia gari la manispaa lililokuwa limetoka kuchukua ushuru kutoka soko la kongowea na kupora takribani shilingi 200,000.

Dereva wa gari hilo amepata majeraha kidogo kichwani yaliyotokana na kukwaruzwa na vyioo vya gari hilo wakati alipikuwa akijaribu kutoroka majambazi hao walipojaribu kumpiga risasi.

Kulingana na dereva wa gari lililovamiwa, Tolbert Ochieng’ alisema kuwa majambazi hao walitoroka wakitumia pikipiki walipotekeleza uhalifu huo.

Afisa mkuu wa Kitengo cha usalama wa kaunti ya Mombasa Charles Karisa alithibitisha tukio hilo siku ya Ijumaa na kusema kuwa uchunguzi utafanyika ili kuwatambua waliotekeleza wizi huo ili hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Aidha alishindwa kuelezea kwa nini gari hilo halikuwa chini ya ulinzi wa polisi kama ilivyo kawaida ya magari yanayosafirisha pesa nchini.