Wizara ya afya ya imepewa changamoto kuhusiana na kujikokota kwake kupambana na funza ambao wamewaathiri maelfu ya watu kote nchini. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu siku ya Jumatano wakati wa kutibu watu ambao wameathiriwa na funza hao hao kule Gesima, mwenyekiti wa shirika la Clean Health Clinton Ouma alihimiza serikali kufanya kazi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kuangamiza funza, huku akiongezea kusema kwamba wizara ya afya hajatekeleza majukumu yake inavyostahili, hali aliyosema imewanyima nafasi wanafunzi kuendeleza ndoto zao shuleni. 

"Tumetembea katika maeneo mengi nchini, na ninaweza thibitisha kwamba wizara ya afya haijafanya ya kutosha kukabiliana na funza kwa kuwa wanafunzi wengi hulazimika kuacha shule kwa kuwa hawawezi tembea vizuri kwenda shuleni, na inastahili serikali kufanya kazi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili kukabiliana na funza hao," alisema Ouma. 

Afisa huyo aidha alizishtumu serikali za kaunti kutokana na kampeni zao za kuangamiza funza kwa kuwa kampeni hizo huwafikia tu watu wa mijini na kuwatenga wale wanaoishi vijijini. 

"Ni kweli kuwa serikali za kaunti zinafanya juhudi kuangamiza funza, ila tu wanazingatia tu maeneo ya kibiashara huku wakiwatenga watu wengine vijijini," alihoji Ouma. 

Shughuli hiyo yakuangamiza funza itawafikia watu wa wadi ya Rigoma na ile ya Gachuba.