Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wizara ya elimu imetoa orodha ya shule ambazo zimesajiliwa katika kaunti ndogo ya Nakuru na tayari orodha hiyo imekabidhiwa manaibu wa chifu.

Tangazo hilo limetolewa na Eunice Khaemba ambaye ni afisa wa elimu katika kaunti ya Nakuru.

Hivyo basi, amewashauri wazazi wanaolenga kuwapaleka watoto wao katika shule yoyote ile kufika kwenye afisi za chifu ili kubaini iwapo shule wanazotaka kuwapeleka wanao zimesajiliwa.

Akizungumza kwenye shughuli ya utoaji wa fedha za ufadhili wa kimasoo na zile za hazina ya Uwezo zilizotolewa katika eneo bunge la Nakuru Magharibi Ijumaa ya tarehe 22 Januari katika uwanja wa Mkarafuu ulio viungani mwa mji wa Nakuru, Khaemba aidha ameonya wanaoanzisha shule bila ya kufuata taraibu zilizotolewa na serikali kwamba hatua hiyo huenda ikaadhiri watoto watakaofika katika shule hizo kupata elimu.

Bi Khaemba anasema kwa kuwapaleka watoto katika shule zilizosajiliwa na wizara ya elimu, wazazi watakuwa na hakikisho kwamba watoto wao watapata elimu bora itakayotolewa na walimu ambao wamepata mafunzo yanayostahili.

Na huku akiangazia makundi ya akina mama waliopata mkopo huo wa hazina ya uwezo, afisa huyo wa elimu kwenye kaunti ndogo ya Nakuru amewataka akina mama hao kutumia fedha hizo kujihamasisha.

Amewataka akina mama hao kama msingi wa taifa na kutumia fedha hizo kwa busara huku pia akiwahimiza kiana mama ambao hawajatafuta fedha hizo kuchukua hatua hiyo ili kuweza kujiendeleza maishani.

Masuala mengine ambayo bi Khameba aliyagusia ni pamoja na ya kuanzishwa kwa shule za bweni katika eneo bunge la Nakuru Mashariki pamoja na lile la baadhi ya watu kutaka kunyakuwa ardhi ya shule huku akishutumu suala hilo.