Share news tips with us here at Hivisasa

Wizara ya usalama wa ndani siku ya Jumatatu ilitangaza kuwafungulia akaunti za WhatsApp waziri Joseph Nkaissery na katibu wa kudumu katika wizara hiyo Karanja Kibicho.

Kulingana na wizara hiyo, nambari ya simu ya 0719777719 itakua ya waziri Nkaissery huku kibicho akitumia 0780719750 katika hatua inayolenga kuboresha mawasiliano baina ya viongozi hao na wananchi.

Hatua hiyo pia inalenga kutoa nafasi kwa wananchi kupata ufafanuzi kuhusu nafasi yao ya kuchangia masuala ya usalama nchini kwa kupata maelezo kutoka kwa maafisa wa usalama.

Wizara hiyo pia imethibitisha kuwa waziri Nkaissery na katibu Kibicho wanapatikana kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, Facebook na Instagram kupitia @GenNkaissery na @kibichokaranja.

Aidha, wananchi wamehimizwa kutoa taarifa muhimu kwa maafisa wa usalama bila kusita ili kusaidia kuthibiti hali ya usalama nchini.

Haya yanajiri baada ya wanajeshi wa KDF kushambuliwa na wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la El Adde nchini Somalia siku kadhaa zilizopita.