Zaidi ya familia ishirini uko kijiji kitwacho Soweto katika mabanda ya Kibera ziliwachwa bila makao baada ya nyumba zao kuteketezwa na moto uliozuka Jumanne asubui, na kuenea kwa kasi kabla ya wakaazi kusaidiana kuuzima kwa maji na mchanga.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza na waandishi wa habari, waadhiriwa walielezea kuwa kuna iwezekano ya kwamba moto huo ulisababishwa na hitilafu za nguvu za umeme.

Wakaazi hao walielezea kuwa wengi wao hawakuweza kuokoa chochote ikiwepo wengine kujeruhiwa vibaya na katika harakati za kuuepuka moto huo.

Chifu wa eneo hilo Bwana Sam Ong'ire aliwaonya wakaazi dhidi ya kuona na kujiekea stima wenyewe, akielezea kuwa kitendo hicho ndicho kimechangia pakubwa katika kuzuka kwa moto katika mabanda hayo. 

"Tatizo la wizi wa umeme limekuwepo kwenye eneo hili la Kibera kwa muda mrefu na nawaonya wote wanaohusika au wanaopanga kuhusika yakwamba kitendo hicho ni halali na kinahatarisha maisha ya wakaazi, na ivyo yeyote atakaye hushishwa na kitendo hicho atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria," alionya Chifu Ong'ire. 

Aidha, wakaazi wa Soweto waliteta kuwa wazima moto huchelewa kila wakati kuna moto kwenye mabanda, Kama ambavyo ilivyofanyika siku hiyo, jambo ambalo husababisha kupotea kwa mali yao kwenye moto.

Wameitaka serikali kuhakikisha kuwa huduma za haraka zaweza kuwafikia bila kuchelewa, wakati wa haja.