Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Zaidi ya wakazi 58,000 katika kaunti ya Mombasa wanaishi na virusi vya Ukimwi.

Hii ni kulingana na takwimu kutoka kwa afisa wa baraza la kuthibiti maambukizi ya Ukiwmi eneo la Pwani Julius Kome.

Uchunguzi huu ulifanywa katika maeneo bunge yote ya kaunti ya Mombasa, ikiwemo eneo bunge la Likoni, Changamwe na Jomvu.

Kome aliyasema haya katika mkutano na wakazi wa Chaani siku ya Alhamisi katika eneo bunge la Changamwe, wakati wakiandaa namna ya kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2015.

Aidha, Kome aliwataka vijana kujitokeza ili kupimwa hali zao za kiafya ili hatua za haraka za kimatibabu kuchukuliwa kwa watakaopatikana na virusi hivyo.

Vile vile, alisistiza kuwa kuna vijana wengi wameambukizwa virusi hivyo, ila hawajajitokeza kujua hali zao kufikia sasa.

Kome aidha aliisihiu jamii kutowatenga wanaoishi na virusi hivyo kwani wao ni binadamu kama wengine.

Katika kikao hicho, mbunge wa eneo la Changamwe Omar mwinyi aliwataka wakazi hao kutojihusisha na ngono kiholela bila kinga ili kuepuka virusi vya ukimwi.