Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Usajili wa wanafunzi wanaohitaji msaada wa karo kupitia basari inayotolewa na serikali ya kaunti ya Nakuru mwaka wa kifedha 2015/16, ulianza rasmi Jumatatu katika wadi ya Bahati.

Zaidi ya wazazi 300 walijitokeza katika ofisi ya mwakilishi wa wadi hiyo.

Aidha kitengo kingine cha wafaidi wa fedha hizo, kitakuwa vijana ambao wanataka kusomea kozi zingine kama uendeshaji magari na kompyuta.

Kulingana na MCA Nderitu, pesa hizo zinanuia kufaidi wale tu ambao ni wanafunzi werevu kutoka familia zisizojiweza.

“Katika utawala uliopita, hata watu walioajiriwa na serikali walikuwa wanaomba basari na kupewa kupitia ufisadi. Mikakati yetu tuliyoweka ni kwamba hakuna mtu kama huyo atapata basari msimu huu," alisema Nderitu.

Baadhi ya wazazi nao walisifia hatua hiyo.

“Afadhali ziwe chache, lakini angalau kila mzazi apate kiasi kidogo cha pesa kumsaidia kulipia karo mwanawe. Tunapongeza MCA Nderitu na pia gavana Mbugua kwa uwazi katika utoaji wa basari hizi,” Milka Wanjiku alisema.