Share news tips with us here at Hivisasa

Ziwa la Nakuru limeorodheshwa miongoni mwa maziwa yenye rangi maridadi zaidi na ya kuvutia macho kwote duniani.

Kwenye orodha iliyotolewa na tovuti la National Geographic, Ziwa la Nakuru liliibuka kwenye nambari ya pili kwote duniani baada ya ziwa la Christmas Island mjini Australia.

Kulingana na orodha iloyotolewa mnamo Alhamisi, National Geographic lilisifu ziwa la Nakuru kuwa lenye rangi maridadi ya kuvutia wageni.

“Maziwa yenye rangi maridadi ya thamani,” National Geographic liliandika kwenye tovuti lao.

“Ziwa la Nakuru lililoko kwenye Bonde kuu la Ufa mjini Kenya, ni makao ya ndege wengi aina ya korongo duniani. Ndege hao wanapokusanyika, wanakaa kama blanketi kubwa lenye rangi la waridi lilotandikwa kwenye ziwa,” National Geographic lilisema.

Miongoni mwa maziwa mengine yaliyoorodhesha na tovuti ni Mallory Square, Key West, Florida; The Lubéron, France; Yellowknife, Northwest Territories, Canada; Erg Chebbi Dunes, Morocco; Grand Prismatic Spring, Wyoming; Caño Cristales, Colombia; Hitsujiyama Park, Japan; Vatnajökull National Park, Iceland

Tovuti la National Geographic linajulikana sana kwa juhudi za kuwahimiza watu kuchunga mazingira tangu mwaka wa 1888.