Wakaazi wa Geteri, eneo bunge la Nyaribaria Masaba, kaunti ya Kisii sasa wanatabasamu, baada ya mradi wa maji kuzinduliwa katika eneo hilo.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongea katika sehemu hiyo siku ya Jumatatu baada ya Scooby International, shirika lisilo la kiserikali kuchimba kisima katika eneo hilo, wakaazi hao walionekana na furaha sana wakidai wamekua wakitembea maili tatu kutafuta maji.

“Susu tunayo furaha sana na tunawapa pongezi wale wote wamehusika kuleta mradi huu, sasa hatutatembea kutafuta maji maeneo mengine bali pia wale walio mbali na mito waje tunayo maji safi yakutumika na kunywa,” alisema Kerubo Monene mkaazi.

Akiwa pia katika maeneo hayo, mwakilishi wadi ya Gesusu Sammy Keronche alisema wananuia kama serikali ya kaunti ya Kisii kuchimba visima Zaidi katika maeneo yote yasiyo karibu na maji katika wadi hiyo

“Kila sehemu iliyoko mbali na maji tunafanya yote yale tunaweza ili kuhakikisha kuwa kila sehemu ya wadi yetu ina maji,” alisema Keronche.

Aidha, aliwataka waakazi hao kuyatumia maji hayo kwa njia nzuri iliyo na manufaa, na sio kwa kujibinafsisha wenyewe.

Pia aliwataka wakaazi hao kuweka mikakati ya kulinda maji hayo ili yadumu bila kuchafuliwa kiholela

Chifu wa lokesheni hiyo amewakaribisha wahisani hao, huku akiwaomba pia kuleta miradhi mingine katika sehemu hiyo

“Tumefurahia sana na karibu tena na miradhi mingine hili mtuwezeshe kuimarisha maisha ya wakaazi hawa tafadhali,” chifu Nyakeruma alisema.